Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya Ballon d’Or baada ya kuwamwaga Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili na Neymer. Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona Neymer akiwa katika pozi. Lionel Messi akiwa akiwa amepozi na Cristiano Ronaldo (kushoto). Neymer akimpongeza Lionel Messi baada ya kuchukua tuzo hiyo. Messi akionesha tuzo hiyo. Kikosi cha XI bora cha FIFA. Messi akisalimiana na Samuel Etoo Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia. Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%. Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake. Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil. Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita. Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia.
Mwanasoka Bora Afrika Kwa Wachezaji Wanaocheza Afrika, Mbwana Ally Samatta alivyo mtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Jana tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Mufti Mkuu mbali na kumpatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko aendako Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi. Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye
HII ni moja ya hekaheka uwanjani kati ya Patrick Vieira and Roy Keane kabla ya mechi ya Arsenal-Manchester United mwaka 2005, na kama kungekuwa na kadi kabla ya mechi kuanza basi hawa jamaa wangekula red card.
Wilfried Zaha akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Crystal Palace dhidi ya Southampton. Cryatal Palace walishinda 2 - 1 katika uwanja wa St Mary's. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Sergio Aguero (kati) akishangilia moja ya goli alilofunga dhidi ya Norwich
MANCHESTER CITY imefanikiwa kushinda mabao 3 - 0 mbele ya Norwich City , katika ushindi huo Sergio Aguero ameweza kufunga mabao mawili na jingine likifungwa na Kevin De Bruyne katika kipindi cha pili.
Lionel Messi ameifungia hat-trick timu yake ya Barcelona dhidi ya Granada katika ushindi wa 4 - 0 na kuiwezesha Barcelona kukaa kileleni mwa msimamo mwa ligi kuu Hispania La Liga .
Messi aliweza kufunga mara mbili ndani ya dakika 14 na baadae alifunga tena dakika ya 58, na goli la nne limefungwa na Neymar dakika ya 83.
Zinedine Zidane akiwa kama kocha mpya wa Real Madrid baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Rafa Benitez . Akizungumza na waandishi wa habari, ametoa msimamo wake juu ya uwezekano wa kuuzwa kwa Cristiano Ronaldo kwamba hawana wazo hilo kwa sasa.
Kocha Mpya Zinedine Zidane akiwa katika majukumu yake mapya kama kocha.
KOCHA Herve Renard wa Ivory Coast ameteuliwa kuwa Kocha Bora barani Afrika. Kocha huyo ameshinda tuzo hiyo katika tamasha la kuwatuza wachezaji bora wa Afrika linaloendelea hivi punde jijini Abuja, Nigeria. Renard raia wa Ufaransa ameteuliwa kuwa kocha bora kutokana na mafanikio yake kwa mwaka 2015. Mpinzani mkubwa kwake alionekana ni Patrice Carteron, hata hivyo hakufua dafu. Kocha huyo ameiwezesha Ivory Coast kubeba ubingwa wa Afrika ikiwa ni mara yake ya pili kufanya hivyo baada ya miaka michache kuwa ameiwezesha Zambia kubeba ubingwa wa Afrika. Lakini Novemba 11, mwaka jana kocha huyo alitimuliwa kazi Lille ya Ufaransa baada ya kuingoza timu hiyo kucheza mechi 13, ikaambulia pointi 13 tu.
Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.
Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani. Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.
Mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku akiifungia timu yake katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup Uwanja wa Goodison Park usiku wa jana. Bao lingine la Everton limefungwa na Ramiro Funes Mori, wakati la City lilifungwa na Jesus Navas
Mbwana Samatta akiwa na kipa Muteba Kadiaba wa TP Mazembe ambaye ameingia naye fainali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika anayecheza soka barani Afrika. Hapa ilikuwa ni punde tu baada ya kuingia ukumbini jijini Lagos, Nigeria.
Nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta akiwa na mshambuliaji nyota wa Borussia Dortmund ya Ujerumani na timu ya taifa ya Gabon, Pierre Aubameyang walipokutana jijini Lagos, Nigeria hivi punde kabla ya kuanza kwa tamasha la kuwatuza wanasoka bora Afrika. Samatta anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika anayecheza soka barani Afrika wakati Aubameyang anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika akichuana na mtetezi wa tuzo hiyo miaka mitatu mfululizo, Yaya Toure na Andre Ayew.
LUIS VAN GAAL alionyesha ishara ya kuaga baada ya mchezo ulioikutanisha Machester United dhidi ya Stoke City katika uwanja wa Britania na Man kupokea kichapo cha 2 - 0. Magoli ya Stoke Yalifungwa na Bojan na Marko Arnautovic.
Southampton 4 - 0 Arsenal Newcastle United 0 - 1 Everton Chelsea 2 - 2 Watford Bournemouth 0 - 0 Crystal Palace Swansea City 1 - 0 West Bromwich Albion Tottenham Hotspur 3 - 0 Norwich City Manchester City 4 - 1 Sunderland Aston Villa 1 - 1 West Ham United Liverpool 1 - 0 Leicester City Stoke City 2 - 0 Manchester United
Kiungo Mkenya wa Southampton, Victor Wanyama akimrukia mchezaji mwenzake Jose Fonte (katikati) na baada ya Martina kufunga jana dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. WASHIKA Bunduki, Arsenal wamepokonywa mtutu na Southampton na kutandikwa risasi nne jana Uwanja wa St Marry’s katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Rhu-Endly Martina alianza kuiadhibu timu ya Arsene Wenger dakika ya 19, kabla ya Shane Long kufunga la pili dakika ya 55 na la nne dakika ya 92, wakati bao la tatu lilifungwa na Jose Fonte dakika 69. Everton imepata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Newcastle United, bao pekee la Tom Cleverley dakika ya 93 Uwanja wa St. James' Park. Chelsea imelazimishwa sare ya 2-2 na Watford mabao yake yote yakifungwa na Diego Da Silva Costa dakika ya 32 na 65, wakati ya wageni yamefungwa na Troy Deeney kwa penalti dakika ya 42 na Odion Ighalo dakika ya 56 Uwanja wa Stamford Bridge. Bournemouth imelazimishwa sare ya 0-0 na Crystal Palace Uwanja wa Vitality, wakati bao pekee la Sung-yueng Ki dakika ya tisa Uwanja wa Liberty limeipa Swansea City ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion. Tottenham Hotspur imeitandika 3-0 Norwich City mabao ya Harry Kane kwa penalti dakika ya 26, dakika ya 42 na Tom Carroll dakika ya 80 Uwanja wa White Hart Lane, wakati Manchester City imeichapa 4-1 Sunderland, mabao yake yakifungwa na Raheem Sterling dakika ya 12, Yaya Toure dakika ya 17, Wilfried Bony dakika ya 22 na Kevin De Bruyne dakika ya 54, wakati la wageni limefungwa na Fabio Borini dakika ya 59 Uwanja wa Etihad.
Kiungo Mspanyola, David Silva akishangilia na mchezaji mwenzake, Raheem Sterling jana Uwanja wa Etihad PICHA ZAIDI BOFYA HAPA Aston Villa imelazimishwa sare ya 1-1 na West Ham United, bao lake likifungwa na Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 62 na Aaron Cresswell dakika ya 47 Uwanja wa Villa Park, wakati bao pekee la Christian Benteke dakika ya 63 limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 Leicester City Uwanja wa Anfield. Stoke City jana ilizidi kumuweka pagumu kocha Mholanzi, Louis Van Gaal baada ya kuichapa Manchester United 2-0, mabao ya Bojan Krkic dakika ya 19 na Marko Arnautovic dakika ya 26 Uwanja wa Britannia.
Christian Benteke (kushoto) akikimbia kushangilia baafa ya kuifungia timu yake bao pekee dhidi ya Leicester jana PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Arnautovic (kushoto) akifumua shuti mbele ya Depay PICHA ZAIDI BOFYA HAPA Kwa matokeo hayo, Leicester City inaendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 38 baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Arsenal pointi 36 za mechi 18, Manchester City poimti 35 za mechi 18 na Tottenham Hotsput pointi 32 za mechi 18 pia.
Kiungo Mkenya wa Southampton, Victor Wanyama akimrukia mchezaji mwenzake Jose Fonte (katikati) na baada ya Martina kufunga jana dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England WASHIKA Bunduki, Arsenal wamepokonywa mtutu na Southampton na kutandikwa risasi nne jana Uwanja wa St Marry’s katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Rhu-Endly Martina alianza kuiadhibu timu ya Arsene Wenger dakika ya 19, kabla ya Shane Long kufunga la pili dakika ya 55 na la nne dakika ya 92, wakati bao la tatu lilifungwa na Jose Fonte dakika 69. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA