Halloween party ideas 2015
Showing posts with label Africa. Show all posts


Pamoja na umahiri wa mtandao wa Wikipedia lakini ajabu umeshindwa kujua uraia wa Mbwana Samatta.

Ile ishu ya wengi duniani kuendelea kuamini Tanzania haiwezi kutoa mwanasoka bora Afrika imeendelea.

Safari hii mtandao wa runinga maarufu ya NBC ya Marekani, wao wamembandika Samatta uraia wa Marekani.

Kupitia mtandao wao wa www.nbcsports.com wameandika Samatta ni mchezaji bora Afrika kwa wanaotokea ndani ya Afrika akiwa anatokea nchini Tunisia!

Kabla ya hapo, mtandao mwingine wa wikipidia nao ulimbandika Samatta uraia wa RD Congo.


Mtandao huo maarufu duniani ulionyesha Samatta ni raia wa DR Congo. Lakini baada ya saa kadhaa ulibadili na kuweka taarifa mpya inayoonyesha kuwa uraia wake ni Tanzania ikiwa ni sehemu ya kurekebisha kosa hilo.


Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.

Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani.

Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.


Nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta akiwa na mshambuliaji nyota wa Borussia Dortmund ya Ujerumani na timu ya taifa ya Gabon, Pierre Aubameyang walipokutana jijini Lagos, Nigeria hivi punde kabla ya kuanza kwa tamasha la kuwatuza wanasoka bora Afrika.

Samatta anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika anayecheza soka barani Afrika wakati Aubameyang anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika akichuana na mtetezi wa tuzo hiyo miaka mitatu mfululizo, Yaya Toure na Andre Ayew.



Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na Mkuu wa Kamati ya Ndani ya Maandalizi (LOC) ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN), Vincent Nzamwita amesema kwamba viwanja vyote vinne vitakavyotumika kwa mashindano hayo, vipo katika hali nzuri tayari kwa mechi.

Michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee, inatarajiwa kuanza Januari 16 hadi Februari 7.
Nzamwita amesema kazi za ukarabati katika viwanja vya Amahoro na Nyamirambo mjini Kigali tayari imekamilika.
Viwanja hivyo ni pamoja na Huye na Umuganda (Rubavu) vitatumika kwa michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika ambayo itashirikisha timu 16 za Afrika.

Mara ya mwisho Rwanda kuandaa mashindano makubwa ya Afrika ilikuwa ni mwaka 2011 ilipokuwa mwenyeji wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Afrika, ambayo mwishoni timu nne ikiwemo Amavubi, ziliiwakilisha Afrika katika fainali za dunia nchini Mexico mwaka huo.


Uwanja wa taifa wa Amahoro ndiyo mkubwa zaidi Rwanda ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 25,000, ukifuatiwa na Huye (mashabiki 10,000), Nyamirambo (mashabiki 7,000) na Umuganda (mashabiki 5,200).
Rwanda imepangwa Kundi A pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gabon, wakati Kundi B lina timu za DRC, Ethiopia, Cameroon na Angola, Kundi C kuna Tunisia, Guinea, Niger na Nigeria na Kundi D kuna Zimbabwe, Zambia, Uganda na Mali


Klabu maarufu sana ya soka nchini Misri imesema kuwa itajiondoa kwenye ligi kuu ya nchini hiyo kutokana na usimamizi mbaya wa mechi.

Klabu ya Zamaleck iliyotwaa ubingwa wa msimu uliopita ilitoa tangazo hilo baada ya kushindwa katika mechi ya jana.
Baraza kuu la klabu hiyo ilikutana baada ya kushindwa mabao 3-2 na klabu ya El-Gaish jumapili usiku na kuamua kutoendelea kutetea taji lao.
Aidha Baraza hilo linatarajiwa kukutana tena jumatatu kujadili jambo hilo.
Shirika la kandanda la Misri limesema halijapokea mawasiliano rasmi kutoka Zamalek.
Pia limetetea vikali viwango vya waamuzi wa ligi hiyo.
Kabla ya mechi hiyo dhidi ya El-Ghaish, Zamalek iliomba refarii Mahmoud Al Banna kubadilishwa kama muamuzi wa mechi lakini ombi hilo lilitupiliwa mbali.
Al Banna alimwonyesha kadi nyekundu mlinzi wa Zamalek Ali Gabr baada ya dakika nne tu na kuwapa El-Gaish penalti.
Refarii huyo aliwatunuku El-Ghaish penalti nyingine katika dakika ya 55.
Kwa mujibu wa sheria za ligi ya Misri, Zamalek wanaweza kuadhabiwa vikali na hata kushushwa daraja ya nne ya ligi wasipobadilisha uamuzi wao.


MIEZI minne baada ya kusaini Mkataba wa miaka mitatu uliogharimu kiasi kisichopungua Sh. Milioni 40, kipa Mudathir Khamis ametemwa klabu ya Yanga SC wiki iliyopita.
Mudathir aliyekuwa analipwa Sh. Milioni 1.3 kwa mwezi, amevunjiwa Mkataba kwa makubaliano ambayo ni siri yake na Yanga SC na amehamia Mgambo JKT ya Tanga.
Kiutaratibu, upande unaoamua kuvunja Mkataba ndiyo hulipa – na malipo anayostahili mvunjiwa Mkataba ni sehemu iliyobaki ya Mkataba wake.
Kwa adhabu kama hizi, tumeona baadhi ya klabu hata Ulaya, zikishindwa kuwavunjia Mikataba wachezaji iliyowapa Mikataba mirefu na kuamua kubaki nao katika timu, ili kukwepa kuwapa fedha nyingi kwa wakati mmoja, ili iwalipe taratibu.

Sasa Yanga wamemlipa kiasi gani cha fedha Mudathir? Ni siri yao. Aidha, Yanga SC wiki mbili zilizopita ilifikia makubaliano ya kuvunja Mkataba na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho akiwa amebakiza karibu mwaka mmoja.
Kimsingi Coutinho naye pia kalipwa. Mwanzoni mwa msimu, wachezaji Hassan Dilunga na Edward Charles pia walivunjiwa mikataba yao, maana yake nao walilipwa.
Aidha, mwanzoni mwa msimu pia, Yanga SC ilimleta beki Joseph Zuttah kutoka Ghana, lakini naye akavunjiwa Mkataba ndani ya mwezi mmoja, kabla ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanza, maana yake naye alilipwa.
Awali ya hapo, Desemba mwaka jana Yanga ilimuacha mshambuliaji Mbrazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’ baada ya nusu msimu.
Baadaye kidogo ikamuacha kiungo Mbrazil, Emerson De Oliviera Neves Roque aliyekuja kuchukua nafasi ya Jaja baada ya wiki tatu akiwa amesaini na kulipwa dau zuri.
Kwa Emerson ilielezwa hakupata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) maana yake huyu inawezekana aliruhusiwa kuondoka tu bila malipo zaidi ya yale ya kusaini.
Na Agosti mwaka huu, Yanga SC imeleta beki Mtogo, Vincent Bossou ambaye amekuja kuanza kucheza baada ya mzalendo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuumia.
Wakati tunasubiri kuona mustakabali wa Bossou, Yanga tena imeleta winga kutoka Niger, Issoufou Boubacar Garba ambaye amesaini Mkataba wa mwaka mmoja.
Yaani inakuwa si shida Yanga kutoa fedha kusajili, au kutoa fedha kumlipa mtu aondoke – maana yake watu hawana uchungu na hizo fedha hata kidogo.
Inafahamika hizo fedha zinatoka kwa mfadhili, ambaye pia ni Mwenyekiti, Yussuf Manji ambaye kwa bahati mbaya yeye hata hajishughulishi sana na timu, hivyo hata kama ‘kupigwa’ atakuwa haelewi chochote.
Watu ambao wanasimamia usajili Yanga wameshindwa kuwa na haya japo kidogo, kufikiria namna wanavyofanya ubadhirifu wa fedha kupitia kivuli cha usajili.
Usajili. Usajili usajili. Usajili imekuwa kama dili ambalo kuna watu ndani ya Yanga wanaomba muda ufike, ili Manji atoe fedha timu isajili na wao ‘wapige chao’.
Hiyo ndiyo dhana ambayo anaweza kuwa nayo mtu yeyote kulingana na hali halisi inayoendelea ndani ya Yanga SC kwa sasa.
Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ makipa wote wanaoaaminiwa wanaelekea kumaliza Mikataba yao na uongozi umemuacha kipa Mudathir badala ya japo kumtoa kwa mkopo kwa kisingizio eti ni mvivu wa mazoezi na ananenepa ovyo.
Jamani kwa waliomuona Mudathir ni kweli amenenepa? Si kweli. Pengine amepungua kuliko wakati anaingia Yanga.
Na suala wa uvivu wa mazoezi kuna adhabu nyingi za kumuadabisha mchezaji, ikiwemo kumkata mshahara au kumpeleka timu ya pili, ili abadilike na kurudi kwenye mstari.
Lakini kwa kumuacha watu wataona tu umetengenezwa mwanya wa dili la kusajili kipa mwishoni mwa msimu ‘zipigwe hela’ tena.
Wakati yote haya yanaendelea, klabu inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo jengo la makao makuu, Jangwani kuwa kama pagala, kutokuwepo kwa Uwanja wa mazoezi na hata msingi imara wa timu ya vijana.
Yanga SC pamoja na kuwa na rasilimaliwatu kubwa, majengo mawili katikati ya mji, bado imeendelea kuwa tegemezi.
Haijulikani viongozi wa Yanga SC wanafanya shughuli gani hata waitwe viongozi – matokeo yake sasa timu inaposafiri kwenye mechi za mikoani hadi walinzi wa ofisi nao wanakwenda.
Ndiyo. Anasafiri Katibu, Mhasibu, Msemaji na wafanyakazi wote wa Ofisi pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji na wote kwa gharama za klabu, kuanzia mafuta ya gari zao, au tiketi za ndege, malazi na posho.
Na hii ni kwa sababu hawana shughuli nyingine za kufanya kuiletea maendeleo Yanga SC na ndiyo maana hata wakati wa mapumziko hulazimisha mechi za kirafiki kwa maslahi yao.
Watu wanafikiria kupata mwanya wa kuchukua hela kwa Mwenyekiti ambaye pia ni Mfadhili, Manji kwa kuzua kambi za mikoani na kadhalika.
Angalau wakati ule wa Lawrence Mwalusako alijitahidi kubana matumizi wakati mwingine wachezaji waliweka kambi makao makuu ya klabu, Jangwani.
Lakini sasa hivi timu inaishi hoteli wakati wote wa msimu – hii watu watafikiria tu ni namna nyingine ya ‘kupiga pesa’ kwa njia ya ‘pasu’ na wenye hoteli.
Yaani ukweli ulivyo Manji ni mtu mwenye moyo wa kipekee wa kuipenda Yanga SC, kwani sina uhakika kama hata bilionea Moise Katumbi Chapwe angeweza kuvumulia mambo kama haya pale TP Mazembe. 
Powered by Blogger.

Powered by themekiller.com