Halloween party ideas 2015
Showing posts with label Michezo Kitaifa. Show all posts

 Mwanasoka Bora Afrika Kwa Wachezaji Wanaocheza Afrika, Mbwana Ally Samatta alivyo mtembelea  Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
 
Jana tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Mufti Mkuu mbali na kumpatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko aendako Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi.
Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye

Simba imefanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, leo.

Bao pekee la Simba katika mchezo huo limefungwa na Jonas Mkude kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi safi ya Emiry Nimuboma raia wa Burundi.

Kutokana na ushindi huo, Simba sasa haitacheza na Yanga, badala yake inakwenda kukutana na Mtibwa Sugar katika mechi ya nusu fainali ya kwanza.

JKU walionyesha soka safi, lakini Simba pia walionekana kuwa katika kiwango kizuri ingawa Said Ndemla na Dani Lyanga walipoteza nafasi nyingi za wazi.


Pamoja na umahiri wa mtandao wa Wikipedia lakini ajabu umeshindwa kujua uraia wa Mbwana Samatta.

Ile ishu ya wengi duniani kuendelea kuamini Tanzania haiwezi kutoa mwanasoka bora Afrika imeendelea.

Safari hii mtandao wa runinga maarufu ya NBC ya Marekani, wao wamembandika Samatta uraia wa Marekani.

Kupitia mtandao wao wa www.nbcsports.com wameandika Samatta ni mchezaji bora Afrika kwa wanaotokea ndani ya Afrika akiwa anatokea nchini Tunisia!

Kabla ya hapo, mtandao mwingine wa wikipidia nao ulimbandika Samatta uraia wa RD Congo.


Mtandao huo maarufu duniani ulionyesha Samatta ni raia wa DR Congo. Lakini baada ya saa kadhaa ulibadili na kuweka taarifa mpya inayoonyesha kuwa uraia wake ni Tanzania ikiwa ni sehemu ya kurekebisha kosa hilo.

KWA mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Mapinduzi, Azam FC imetolewa katika hatua ya makundi, baada ya kufungwa mabao 2-1 jioni ya leo na Mafunzo FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Azam FC pia inaondoka bila ya ushindi katika mashindano hayo, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia yake ya ushiriki wa michuano hiyo ikimaliza na pointi mbili, za sare dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar, zote 1-1 pamoja na kipigo cha leo. 

Aliyewarudisha mapema Azam FC Dar es Salaam leo ni Habib Sadik aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Haji Abdi dakika ya 90 na ushei kuipatia Mafunzo bao la pili.
Azam FC walitangulia kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Kipre Herman Tchetche dakika ya 20 akimalizia kona iliyochongwa na beki wa kulia, Shomary Kapombe.
Mshambuliaji wa Azam FC akimtoka beki wa Mafunzo, Abdulaziz Makame wa Mafunzo
Mafunzo ambao leo walicheza bila kocha wao Mkuu, Hemed Morocco, aliyefiwa na mama yake mzazi, ilipata bao la kusawazisha dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake, Rashid Abdallah  aliyemalizia pasi ya Ali Hassan.
Matokeo haya yanazifanya Yanga SC na Mtibwa Sugar zenye pointi nne kila moja zifuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali na zitamenyana katika mechi ya mwisho ya kundi A usiku wa leo kusaka mshindi wa kwanza na wa pili.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Ivo Mapunda, Shomary Kapombe/Khamis Mcha dk 79, Erasto Nyoni, Serge Wawa, Abdallah Kheri, Farid Mussa/Ramadhani Singano dk65, Abubakar Salum, Mudathir Yahaya/Frank Domayo dk65, Allan Wanga, Kipre Bolou/Ame Ali dk69 na Kipre Tchetche.
Mafunzo; Khalid Haji, Juma Mmanga/Kheri Salum dk 10, Haji Mwambe, Haji Hassan, Said Shaaban, Ali Hassan/Jermaine Seif dk58, Samih Nuhu/Ahmed Maulid dk84, Hassan Juma, Abdulaziz Makame, Rashid Abdallah na Shaaban Ali/Sadick Habib dk72.
Kipre Tchetche akienda hewani kuifungia Azam FC bao kuongoza 

YANGA SC imemaliza kileleni mwa Kundi B michuano ya Kombe la Mapinduzi, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na kutoa sare moja, hivyo kuongoza Kundi B ikifuatiwa na Mtibwa inayomaliza na pointi nne, Mafunzo pointi tatu, wakati Azam FC waliovuna pointi mbili wameshika mkia na kuaga.
Yanga SC sasa itacheza na mshindi wa pili wa Kundi A katika Nusu Fainali, wakati Mtibwa Sugar itacheza na mshindi wa pili wa kundi hilo.
Mtibwa Sugar walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wake, Shizza Kichuya aliyemalizia pasi ya mshambuliaji anayecheza kwa mkopo timu hiyo ya Manungu kutoka Yanga SC, Hussein Javu.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma (kulia) akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde



Malimi Busungu (kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Yanga SC bao la ushindi

Yanga SC walisota hadi dakika ya 42 walipofanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa kiungo wake mpya kutoka Niger, Boubacar Issoufou.
Issoufou alifunga bao hilo kwa shuti zuri la mpira wa adhabu kutoka pembeni kulia nje kidogo ya boksi, baada ya mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma kuangushwa na beki wa Mtibwa, Salum Mbonde.
Kwa ujumla, kipindi cha kwanza timu zote zilicheza vizuri, Mtibwa Sugar wakitawala sehemu ya kiungo na Yanga SC wakipitisha mashambulizi yao pembezoni mwa Uwanja.
Kipindi cha pili, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini mwishowe bahati ilikuwa ni ya Yanga waliofanikiwa kushinda mechi.
Mshambuliaji Malimi Busungu aliyetokea benchi, aliwafungia mabingwa hao wa Bara bao la pili dakika ya 81 akimalizia krosi ya winga Simon Msuva.
Kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph aliyetokea benchi kipindi cha pili, alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwishoni baada ya kumchezea rafu Salum Telela.
Mechi za makundi zinatarajiwa kuhitimishwa kesho kwa michezo ya Kundi A, kati ya URA na Jamhuri jioni na Simba SC na JKU usiku.
Hadi sasa, Simba SC inaongoza Kundi A kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na URA na JKU zenye pointi tatu kila moja.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan/Pato Ngonyani dk89, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Salum Telela dk74, Donald Ngoma/Paul Nonga dk65, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk56 na Boubacar Issoufou/Boubacar Issoufou dk71.
Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Andrew Vincent/Dickson Daud dk10, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Hussein Javu/Said Bahanuzi dk63, Ibrahim Rajab ‘Jeba’/Henry Joseph dk76 na Vincent Barnabas/Mohamed Ibrahim dk56.

Nahodha wa Azam FC amewaomba radhi mashabiki wa kikosi hicho kutokana na kuboronga katika michuano ya Mapinduzi.

Azam FC imetolwa hatua ya makundi baada ya kushika mkia katika Kundi B kwa kutoka sare mbili na kupoteza mchezo mmoja hivyo kubaki na pointi mbili tu. Haya ndiyo maneno ya Bocco aliyoyatupia kwenye mtandao wa kijamii.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki wote wa Azam Fc kwa performance mbaya tulioonyesha kwenye mashindano ya Mapinduzi na mechi mbili za Ligi kabla ya kuja huku, matokeo ni sehemu ya mchezo inakubalika, lakin kitu kinacho angaliwa ni unapataje matokeo yawe mazuri au mabaya.

"Tumepata matokeo mabaya kutoka kwenye performance mbaya zaidi kuwahi kuiona katika timu yetu tangu nilipoanza kucheza hadi sasa hivi, hivo tunawaomba radhi mashabiki wetu wote na kuwaaidi tutajituma na kupigania club yetu kwa moyo wetu wote."


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo baada ya kuomba kwa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu  nchini (TFF).

Kaijage aliiongoza Twiga Stars kwenye fainali za michezo ya Afrika (All Africa Games) zilizofanyika nchini Congo Brazzavile Septemba mwaka jana, baada ya kuiondoa timu ya taifa ya Zambia katika hatua ya mtoano.

TFF imesikitishwa na taarifa za kujiuzulu kwa kocha huyo mwenye leseini A ya CAF, ambaye amekuwa akizinoa timu za taifa za wanawake ya wakubwa (Twiga Stars) pamoja na timu ya wanawake wenye umri chini ya miaka ya 20 (Tanzanite) tangu mwaka 2013.

Kufuatia kujiuzulu kwa kocha Kaijage, TFF inaendelea na programu za maendeleo ya soka kwa wanawake, ikiwemo kuendesha ligi ya wanawake (Tanzania Women League).

TFF inamtakia kila la kheri kocha Rogasian Kiajage katika shughuli zake.

Aidha maandalizi ya mchezo kati ya Twiga Stars dhidi ya Zimbambwe  yataendelea chini ya kocha atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, mchezo utakaochezwa mwezi Machi mwaka huu na mshindi kucheza na Zambia.

Yanga imeitwanga Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 na kukaa kileleni Kundi B katika michuano ya Mapinduzi.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi sasa inasubiri mshindi wa pili kundi A lenye timu za Simba, JKU, URA na Jamhuri.

Katika mechi ya leo, Mtibwa Sugar ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya katika dakika ya 10 kabla ya Yanga kusawazisha kupiitia Issoufou Boubacar katika dakika ya 42.

Boubacar alifunga bao safi la mkwaju wa adhabu, pembeni kabisa na kuamsha shamrashamra kwa mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Timu hizo zilikwenda mapumziko kwa sare ya 1-1 na baada ya hapo ilikuwa ni kushambuliana kwa zamu huku Yanga ikionekaan kuimarika zaidi baada ya kuwaingiza Salum Telela, Malimi Busungu na Paul Nonga.

Yanga ilipata bao la pili kupitia Malimi Busungu katika dakika ya 82 akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva na mabeki wa Mtibw Sugar wakamsahau hivyo kupata nafasi ya kupiga kichwa akiwa peke yake na mpira ukamshida kipa Said Mohammed Mduda.

Mkongwe Henry Joseph aliyeingia, alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo Telela.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC.

 Hajji Sunday Manara akiwa mbele ya gari aina ya Range Rover Sport nyekundu katika eneo la kuegeshea magari yanayouzwa. Haikujulikana mara moja kama mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara 'Kompyuta' alikuwa anataka kununua gari hilo, au amepiga picha tu. Hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alimtambia Hajji kwamba yeye anaendesha gari zuri ambalo Ofisa huyo wa Simba SC hana. Tuseme Hajji anataka kumjibu Jerry Muro?

Wachezaji wa Yanga SC wakifurahia bao lao la tatu leo dhidi ya Mbeya City

YANGA SC imetanua mbawa kileleni mwa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 33, baada ya kucheza mechi 13, wakati Azam FC iliyocheza mechi 12, ina pointi 29.

Mrundi Amissi Tambwe aliifungia Yanga SC mabao mawili mfululizo, la kwanza dakika la 37 akimalizia pasi ya winga Simon Msuva na la pili dakika ya 65 akimalizia krosi ya Mwinyi Hajji Mngwali, kabla ya kumpasia kwa kichwa Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tatu dakika ya 
66.



Katibu Mkuu wa Chama cha Soka visiwani Zanzibar Kassim Haji Salum amesema Klabu za Gor Mahia ya kenya , KCCA ya Uganda , Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa sugar kutoka Tanzania Bara na Mafunzo na JKU kutoka visiwani Zanzibar ndio Timu zitakazoshiriki Mashindano ya Mapinduzi Cup Mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza Januari 2 visiwani Humo.

Michuano ya Mapinduzi Cup itazisaidia Timu za Yanga, Azam FC, JKU na Mafunzo kujiandaa na Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika.
Yanga watacheza michuano ya CAF Champion Ligi kwa kucheza mchezo wa mtoano na Timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius wakati Azam FC watacheza na Mshindi kati ya Klabu ya Seychelles na Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika Kombe la Shirikisho.

Mafunzo ya zanzibar wao watacheza na klabu ya AS Vita ya Congo DR kwenye CAF Champion Ligi na Timu ya JKU itashiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Gaborone United ya Botswana.


Kikosi cha Simba SC kilichofungwa 3-1 na Geita Gold Mine inayofundishwa na kocha Suleiman Matola, katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa shule ya Wajja Spring, Geita. Kutoka kulia kocha Dylan Kerr, Awadh Juma, Joseph Kimwaga, Paul Kiongera, Brian Majwega, Said Issa, Hajji Ugando, Daniel Lyanga, Novat Lufunga, Emery Nimubona na Mohammed Fakhi. Aliyechuchumaa mbele ni kipa Peter Manyika.


Straika nyota wa Stand United ya Shinyanga, Elias Maguri, amedai kuwa muda wowote kuanzia sasa anaweza kuikacha klabu hiyo kama hali ya utulivu itaendelea kupotea.

Stand United hivi sasa inakabiliwa na matatizo makubwa ya utulivu kutokana na viongozi wake kila wakati kuvurugana jambo ambalo limeanza kuigawa timu hiyo katika makundi tofauti.

Maguri alisema vurugu hizo za viongozi hao zimechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kupoteza mechi zake mbili za Ligi Kuu Bara ilizocheza hivi karibuni dhidi ya Mwadui FC na Yanga.

“Wachezaji hivi sasa wameanza kugawanyika katika makundi wakiwaunga mkono baadhi ya viongozi wanaowaamini.

“Hali hiyo ndiyo hasa imechangia tushindwe kufanya vizuri katika mechi mbili zilizopita kwa sababu ushirikiano uliokuwepo uwanjani hivi sasa haupo tena kila mtu anacheza anavyojua yeye.


“Kama hali hii itaendelea hivi hakuna haja ya kuendelea kuumiza kichwa na timu hii inabidi tutafute njia nyingine za kufanya kwa sababu yote haya wameyataka wao,” alisema Maguli ambaye kwa sasa anaongoza kwa kuzifumania nyavu akiwa na mabao tisa mbele ya Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma.


MTIFUANO uliokuwa ukiendelea baina ya Simba na kiungo wao, Mzimbabwe, Justice Majabvi umefikia ukingoni baada ya pande hizo mbili kumaliza tofauti zao na mchezaji huyo tayari amesharejea kundini.

Majabvi na uongozi wa timu hiyo waliingia kwenye mtafaruku mkubwa wiki iliyopita baada ya kiungo huyo kueleza kukerwa kuishi kwenye hoteli huku akidai kuhitaji nyumba, kingine jinsi mambo yalivyokuwa yakienda klabuni hapo na mazingira ya kambi kuwa mabaya.

Hata hivyo, imeelezwa kwamba, mchezaji huyo amezungumza na baadhi ya viongozi wa timu hiyo, mambo yamekaa sawa na akapewa sharti la kuandika barua ya kuomba radhi kisha akajiunge na wenzake mkoani Shinyanga wanakojiandaa na mechi ya Mwadui FC itakayopigwa Jumamosi hii.

Katika suala la kukatwa mshahara kwa kiungo huyo ikiwa kama adhabu yake, hiyo pia imefafanuliwa kuwa viongozi wengi hawaungi mkono suala hilo, hivyo bado kuna mvutano mpaka hapo kitakapofanyika kikao cha pamoja na kukubaliana.

“Mambo yako poa sasa, Majabvi alikutana na baadhi ya viongozi, wakazungumza na mambo yamekwisha ila ameambiwa aandike tu barua ya kuomba radhi ambayo alitakiwa kuikabidhi leo (jana) asubuhi kisha achukue ndege aiwahi timu Shinyanga.


“Kuhusiana na ile ishu ya kukatwa mshahara, hiyo nayo haina nguvu sana maana hakuna kikao kilichopitisha na wengi hawaungi mkono,” alisema moja ya vigogo wa timu hiyo.


TIMU ya Simba SC imelazimishwa kutoka suluhu ya magoli 1 - 1 na Toto Africans , katika mfululizo wa michezo ya Vodacom Premier League,VPL.
Simba ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mshabuliaji wake mpya aliyekuwa anaichezea FC Lupopo Ya DRC Dany Lyanga katika kipindi cha kwanza.

Lakini Toto Africans waliweza kurejesha bao hilo katika dakika za nyongeza dkk 90+1.

Amissi Tambwe akishangilia baada ya kufunha hat trick leo Yanga ikishinda 4-0

YANGA SC imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unawafanya mabingwa hao watetezi wafikishe pointi 30 baada ya kucheza mechi 12, wakiizidi pointi nne Azam FC ambayo ina mechi mbili mkononi. 
Shujaa wa Yanga SC leo alikuwa ni Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe aliyefunga mabao peke yake, wakati bao lingine limefungwa na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
Tambwe alifunga mara tatu mfululizo kipindi cha kwanza, dakika ya 20 akimalizia pasi nzuri ya kiungo Thabani Kamusoko, dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa Juma Abdul na dakika ya 45 akimalizia pasi ya Mzimbabwe Donald Mgoma.
Katika kipindi hicho, Stand United walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga dakika ya 30 Elias Maguri alipiga nje na dakika ya 44 Haroun Chanongo aligongesha mwamba kipa Deo Munishi ‘Dida’ akiwa amekwishapotea.
Kamusoko aliifungia Yanga SC bao la nne dakika ya 63 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Juma Abdul aliyekuwa katika kiwango kizuri leo.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Bossou, Kelvin Yondani/Pato Ngonyani dk78, Said Juma, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Matheo Anthony dk74, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk78. 
Stand United; Frank Muwonge, Nassor Said ‘Chollo’, Abuu Ubwa/Suleiman Mrisho dk78, Revocatus Richard, Philip Metusela, Jacob Massawe, Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Jeremiah Katula dk67, Elias Maguri, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Erick Kayombo.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Simba SC imelazimishwa sare ya 1-1 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Simba SC walianza kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa Danny Lyanga kabla ya Salmin Hoza kuisawazishia Toto dakika ya 86.
Mechi nyingine za leo, Mwadui FC imeifunga 2-1 Ndanda FC, Kagera Sugar imeifunga 1-0 African Sports, Prisons imelazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi tatu, Majimaji na Azam FC ambayo awali ilikuwa ifanyike leo mjini Songea, JKT Ruvu na Coastal Union na Mbeya City na Mgambo JKT.
Powered by Blogger.

Powered by themekiller.com