Straika nyota wa Stand United ya Shinyanga, Elias Maguri, amedai kuwa muda wowote kuanzia sasa anaweza kuikacha klabu hiyo kama hali ya utulivu itaendelea kupotea.
Stand United hivi sasa inakabiliwa na matatizo makubwa ya utulivu kutokana na viongozi wake kila wakati kuvurugana jambo ambalo limeanza kuigawa timu hiyo katika makundi tofauti.
Maguri alisema vurugu hizo za viongozi hao zimechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kupoteza mechi zake mbili za Ligi Kuu Bara ilizocheza hivi karibuni dhidi ya Mwadui FC na Yanga.
“Wachezaji hivi sasa wameanza kugawanyika katika makundi wakiwaunga mkono baadhi ya viongozi wanaowaamini.
“Hali hiyo ndiyo hasa imechangia tushindwe kufanya vizuri katika mechi mbili zilizopita kwa sababu ushirikiano uliokuwepo uwanjani hivi sasa haupo tena kila mtu anacheza anavyojua yeye.
“Kama hali hii itaendelea hivi hakuna haja ya kuendelea kuumiza kichwa na timu hii inabidi tutafute njia nyingine za kufanya kwa sababu yote haya wameyataka wao,” alisema Maguli ambaye kwa sasa anaongoza kwa kuzifumania nyavu akiwa na mabao tisa mbele ya Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma.
Post a Comment