Halloween party ideas 2015


MTIFUANO uliokuwa ukiendelea baina ya Simba na kiungo wao, Mzimbabwe, Justice Majabvi umefikia ukingoni baada ya pande hizo mbili kumaliza tofauti zao na mchezaji huyo tayari amesharejea kundini.

Majabvi na uongozi wa timu hiyo waliingia kwenye mtafaruku mkubwa wiki iliyopita baada ya kiungo huyo kueleza kukerwa kuishi kwenye hoteli huku akidai kuhitaji nyumba, kingine jinsi mambo yalivyokuwa yakienda klabuni hapo na mazingira ya kambi kuwa mabaya.

Hata hivyo, imeelezwa kwamba, mchezaji huyo amezungumza na baadhi ya viongozi wa timu hiyo, mambo yamekaa sawa na akapewa sharti la kuandika barua ya kuomba radhi kisha akajiunge na wenzake mkoani Shinyanga wanakojiandaa na mechi ya Mwadui FC itakayopigwa Jumamosi hii.

Katika suala la kukatwa mshahara kwa kiungo huyo ikiwa kama adhabu yake, hiyo pia imefafanuliwa kuwa viongozi wengi hawaungi mkono suala hilo, hivyo bado kuna mvutano mpaka hapo kitakapofanyika kikao cha pamoja na kukubaliana.

“Mambo yako poa sasa, Majabvi alikutana na baadhi ya viongozi, wakazungumza na mambo yamekwisha ila ameambiwa aandike tu barua ya kuomba radhi ambayo alitakiwa kuikabidhi leo (jana) asubuhi kisha achukue ndege aiwahi timu Shinyanga.


“Kuhusiana na ile ishu ya kukatwa mshahara, hiyo nayo haina nguvu sana maana hakuna kikao kilichopitisha na wengi hawaungi mkono,” alisema moja ya vigogo wa timu hiyo.

Post a Comment

Powered by Blogger.

Powered by themekiller.com