Halloween party ideas 2015

Manchester City wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea City, wakipata bao kupitia mpira uliopigwa na Yaya Toure dakika za mwisho.
Dalili zote zilikuwa zimeonyesha kana kwambwa wangeondoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wageni wao, lakini Bafétimbi Gomis akasawazisha dakika za mwisho. Lakini mambo yalikuwa bado kwani kulikuwa bado na muda kwa Toure kugongesha mpira kwenye mgongo wa Kelechi Iheanacho, na mpira huo ukamkwepa Lukasz Fabianski na kuingia wavuni.
Bao la kwanza la City lilifungwa na Wilfried Bony.

Post a Comment

Powered by Blogger.

Powered by themekiller.com