Kelechi Iheanacho |
MSHABULIAJI wa Manchester City Kelechi Iheanacho ni mmoja kati ya wachezaji waliojumuishwa katika kikosi cha Super Eagle kitakacho wavaa Misri kuwania kufuzu fainali za Afrika.
Kocha wa Super Eagle Samson Siasia pia amemjumuisha Victor Moses kutoka West-Ham, Odion Ighalo kutoka Watford, John Mikel Obi wa Chelse na Alex Iwobi wa Arsenal. Kocha Samson Siasia ni kocha wa muda kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sunday Oliseh
Nigeria iliyopo kundi G itavaana na Misri tarehe 25 machi 2016 mjini Kaduna,Nigeria na baadae tarehe 29 March 2016 watacheza mechi ya marudiano mjini Alexandria,Misri
Nigeria yenye pointi mbili nyuma ya vinara wa kundi hilo Misri watatakiwa kushinda mechi zao ili kujihakikishia nafasi,kwani mshindi wa kila kundi atakuwa amefuzu moja kwa moja kuelekea Gabon zitakazo fanyika fainali hizo.
Kelechi Iheanacho aliyecheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Swaziland, ameitwa kutokana kuwa na uwiano mzuri wa magoli alifunga akichezea vilabu vya England msimu huu.
Alex Iwobi miaka-19 aliyechezea timu ya vijana ya Uingereza ameitwa kwa mara nyingine baada ya kujumuishwa katika mechi za DR Congo na Cameroon katika mechi za kirafiki, huyu ni mpwa wa aliyekuwa kapteni wa Nigeria Austin Jay-Jay Okocha.
Kiungo wa Lazio ya Italia Ogenyi Onazi hatacheza mchezo utakaofanyika mjini Kaduna kutokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Chad June 2015.
Sasia amewajumuisha wachezaji wa ndani walioiongoza Nigeria kutwaa ubingwa wa U-23 mwaka jana ambao ni Azubuike Okechukwu, Usman Mohammed and Etebo Oghenekaro
Siasia ataanza kambi na wachezaji wa ndani mwishoni mwa wiki hii mjini Abuja.
Kikosi Cha Nigeria:
Goalkeepers: Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England); Daniel Akpeyi (Chippa United, SA)
Defenders: Abdullahi Shehu (Uniao da Madeira, Portugal); Elderson Echiejile (AS Monaco, France); Kenneth Omeruo (Kasimpasa, Turkey); Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Turkey); Efe Ambrose (Celtic FC, Scotland); Staneley Amuzie (Olhanense, Portugal)
Midfielders: Ogenyi Onazi (SS Lazio, Italy); John Mikel Obi (Chelsea FC, England); Azubuike Okechukwu (Yeni Malatyaspor, Turkey), Victor Moses (West Ham United, England)
Forwards: Ahmed Musa and Aaron Samuel (CSKA Moscow, Russia); Moses Simon (KAA Gent, Belgium); Odion Ighalo (Watford FC, England); Alex Iwobi (Arsenal FC, England); Fanendo Adi (Portland Timbers, USA), Aminu Umar (Osmanlispor, Turkey), Kelechi Iheanacho (Manchester. City, England)
Wachezaji Wa Ndani:
Ikechukwu Ezenwa, Femi Thomas, Austin Oboroakpo, Kalu Orji, Chibuzor Okonkwo, Etim Matthew, Sincere Seth, Segun Oduduwa, Chima Akas, Chris Madaki, Oke Ogagatewho, Ifeanyi Matthew, Usman Mohammed, Etebo Oghenekaro, Stanley Dimgba, Yau Hassan, Ezeikel Bassey, Prince Aggreh, Bright Onyedikachi, Chisom Chikatara, Godwin Obaje, Emmanuel Daniel
Post a Comment