Halloween party ideas 2015


MWANARIADHA Oscar Pistorius aliyepatikana kwa kosa la mauaji ya aliyekuwa Mpenzi wake Reeva Steenkamp mnamo February 2013 baada ya kumpiga risasi nne kupitia mlango wa choo.
Mahakama imesikiliza rufaa na utetezi wa mbande zote mbili na inategemea kutoa uamuzi wake mwezi wa nne(18-April 2016) mwaka huu mbele ya Jaji Thokozile Masipa

Hatua hii itawapa nafasi mawakili wa pande zote mbili kujadili urefu wa adhabu atakayopewa mshitakiwa,Pistorius 


Kelechi Iheanacho
MSHABULIAJI wa Manchester City Kelechi Iheanacho ni mmoja kati ya wachezaji waliojumuishwa katika kikosi cha Super Eagle kitakacho wavaa Misri kuwania kufuzu fainali za Afrika.

Kocha wa Super Eagle Samson Siasia pia amemjumuisha Victor Moses kutoka West-Ham, Odion Ighalo kutoka Watford, John Mikel Obi wa Chelse na Alex Iwobi  wa Arsenal. Kocha Samson Siasia ni kocha wa muda kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sunday Oliseh

Nigeria iliyopo kundi G itavaana na Misri tarehe 25 machi 2016 mjini Kaduna,Nigeria na baadae tarehe 29 March 2016 watacheza mechi ya marudiano mjini Alexandria,Misri

Nigeria yenye pointi mbili nyuma ya vinara wa kundi hilo Misri  watatakiwa kushinda mechi zao ili kujihakikishia nafasi,kwani mshindi wa kila kundi atakuwa amefuzu moja kwa moja kuelekea Gabon zitakazo fanyika fainali hizo.

Kelechi Iheanacho aliyecheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Swaziland, ameitwa kutokana kuwa na uwiano mzuri wa magoli alifunga akichezea vilabu vya England msimu huu.

Alex Iwobi miaka-19 aliyechezea timu ya vijana ya Uingereza ameitwa kwa mara nyingine baada ya kujumuishwa katika mechi za DR Congo na Cameroon katika mechi za kirafiki, huyu ni mpwa wa aliyekuwa kapteni wa Nigeria Austin Jay-Jay Okocha.

Kiungo wa Lazio ya Italia Ogenyi Onazi hatacheza mchezo utakaofanyika mjini Kaduna kutokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Chad June 2015.

Sasia amewajumuisha wachezaji wa ndani walioiongoza Nigeria kutwaa ubingwa wa U-23 mwaka jana ambao ni Azubuike Okechukwu, Usman Mohammed and Etebo Oghenekaro

Siasia ataanza kambi na wachezaji wa ndani mwishoni mwa wiki hii mjini Abuja.

Kikosi Cha Nigeria:

Goalkeepers: Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England); Daniel Akpeyi (Chippa United, SA)

Defenders: Abdullahi Shehu (Uniao da Madeira, Portugal); Elderson Echiejile (AS Monaco, France); Kenneth Omeruo (Kasimpasa, Turkey); Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Turkey); Efe Ambrose (Celtic FC, Scotland); Staneley Amuzie (Olhanense, Portugal)

Midfielders: Ogenyi Onazi (SS Lazio, Italy); John Mikel Obi (Chelsea FC, England); Azubuike Okechukwu (Yeni Malatyaspor, Turkey), Victor Moses (West Ham United, England)

Forwards: Ahmed Musa and Aaron Samuel (CSKA Moscow, Russia); Moses Simon (KAA Gent, Belgium); Odion Ighalo (Watford FC, England); Alex Iwobi (Arsenal FC, England); Fanendo Adi (Portland Timbers, USA), Aminu Umar (Osmanlispor, Turkey), Kelechi Iheanacho (Manchester. City, England)

Wachezaji Wa Ndani:
Ikechukwu Ezenwa, Femi Thomas, Austin Oboroakpo, Kalu Orji, Chibuzor Okonkwo, Etim Matthew, Sincere Seth, Segun Oduduwa, Chima Akas, Chris Madaki, Oke Ogagatewho, Ifeanyi Matthew, Usman Mohammed, Etebo Oghenekaro, Stanley Dimgba, Yau Hassan, Ezeikel Bassey, Prince Aggreh, Bright Onyedikachi, Chisom Chikatara, Godwin Obaje, Emmanuel Daniel

TIMU ya LEICESTER CITY ikiwa na matumaini ya kutanua uwingo wa pointi tano 5 nyuma ya Tottenham HotSpur yenye point 54 katika nafasi ya zilififia pale walipotoka suluhu ya mabao ya 2 -2 na WEST-BROM.
Katika mchezo huo WEST BROM ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 kupitia kwa Salomon Rondon, lakini Magoli ya Danny Drinkwater na Andy King yaliifanya LEICESTER CITY kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 2 -1.

Wakiwa na matumaini ya kutoka na pointi zote tatu, Craig Gardner alihaaribu plani ya LEICESTER kwa kuizawazishia WEST BROM, na mapaka dakika ya 90 mabao yalikuwa 2 -2.

Craig Gardner (kulia) akishangilia baada ya kuifingia West Brom goli la pili dhidi ya Leicester City Jumanne usiku

Craig Gardner (kushoto) akiizawazishia WEST BROM katika dakika ya 50 dhidi ya Leicester City Jumanne usiku

Craig Gardner (katikati) akipongezwa na wenzake baada kuzawazisha goli kwa mkwaju wa adhabu.

Craig Gardner  akishangilia baada ya kuifingia West Brom goli kwa mkwaju wa adhabu dhidi ya Leicester City Jumanne usiku













 Watumiaji wa programu za michezo ya kielektroniki wanawataka watengenezaji wa mchezo wa FIFA 2016 kuimarisha hadhi ya mchezaji chipukizi wa Manchester United , Marcus Rashford.
Shinikizo hilo linafuatia mwanzo wenye ufanisi mkubwa katika mechi zake za ligi kuu ya uropa na ile ya uingereza dhidi ya Arsenal ambapo kijana huyo alifunga mabao mawili.
Kulingana nao mchezaji huyo aliyefufua matumaini ya Manchester United msimu huu anapaswa kutambuliwa na kupewa hadhi ya juu anayostahili katika programu hiyo ya FIFA 2016.
Kocha wa Man United Louis Van Gaal alimsifu kwa ''kipaji chake cha kipekee''.
Hata kocha wa timu hasimu Arsenal, Arsene Wenger alitamaushwa na uwezo na uweledi wa chipukizi huyo machachari aliyefuma mabao mawili ya kwanza dhidi yao siku ya jumapili.
Sasa mashabiki wake wanataka kampuni inayoitengeneza programu hiyo waimarishe hadhi yake.
Kampuni hiyo ya EA Sports, huwa inamuorodhesha mchezaji yeyote na kutathmini ubora wake na kumpa alama juu ya 100% ima ni ushambuliaji kasi na uwezo wake wa kufunga mabao.
Katika programu hiyo kwa sasa Rashford amepewa hadhi ya mchezaji wastani na jumla ya alama 59 (ambayo sio nzuri ya kutosha kwa mujibu wa wafuasi wa klabu hicho cha Manchester United).
Aidha Rashford anagharimu takriban pauni laki tatu pekee (300,000) katika soko hilo la kielektroniki ambalo huendeshwa kwa njia sawa na soko la wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza.
Mmiliki mmoja wa programu hiyo ya FIFA 2016 ernie_els alichapisha hoja kwenye mitandao akidai kuwa ''Rashford ndiye mshambuliaji nyota katika ligi kuu ya Uingereza kwa sasa'' Aidha alimfananisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 na Ronaldo na kumbatiza jina "Rashaldo".
Vilevile EA Sports walishauriwa moja kwa moja : "Kufanya lisilobudi yaani,kuimarisha hadhi yake kulingana na matokeo yake uwanjani kwa kumpa alama za juu zaidi takriban asilimia 65% jumla na asilimia 70% katika ushambuliaji na umahiri wake.

''Aidha kasi yake ikitathminiwa kuwa kati ya 77-78% huku ubora wake ukikisiwa kupanda hadi kati ya asili mia 82-83''.
Mikey Kalinowski naye alisema kuwa ''kwa kweli ni mapema mno kumsawazisha na kigogo wa soka ya Argentina na Barcelona ya Uhispania Lionel Messi.
Hata hivyo aliendelea kusema kuwa Rashford ni mbora kumzidi Messi''
Hayo yote ni kenda mpenzi msomaji tuachie maoni yako kuhusu ripoti hii kupitia mitandao yetu ya kijamii katika Facebook Twitter na Instagram.


Bingwa wa michezo ya ndani kwa ndani katika mbio za mita 1500 Abeba Aregawi amesimamishwa kwa mda kushiriki katika mchezo huo baada ya kupatikana na dawa za kisisimua misuli.

Mwanariadha huyo wa Ethiopia aliyezaliwa nchini Sweden mwenye umri wa miaka 25 alipatikana na dawa hiyo baada ya kufanyiwa kipimo na shirikisho la riadha duniani IAAF.
Abeba alikimbilia Ethiopia katika michezo ya Olimpiki ya 2012 lakini akaanza kuiwakilisha Sweden baadaye mwaka huo baada ya kupewa uraia.

Marufuku yake inamaanisha kwamba nafasi yake katika kikosi cha Sweden katika mashindano ya Olimpiki ina utata.
Kamati ya Olimpiki ya Sweden tayari imeondoa ufadhili wake kwa mwanariadha huyo.

Arsenal hawana budi kusahau kichapo cha Manchester United na kuganga ya Swansea.
Mkufunzi wa klabu hicho Arsene Wenger anasema kuwa kichapo hicho cha 3-2 uwanjani Old Trafford hakifai kuwadumaza washika bunduki hao kwani nia na azimio la ni kukata kiu cha kombe la ligi kuu ya Uingereza.
Arsenal wamesalia katika nafasi ya 3 lakini sasa wana alama 5 nyuma ya vinara wa msimu huu Leicester.

Tottenham walijifurukuta na kuibana Swansea 2-1 na kusalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 54 tatu zaidi ya The Gunners.
''Kwa hakika hatuwezi kujihurumia eti kwa sababu tuliambulia kichapo Old Trafford ,lazima tujifurukute na kuthibitishia wapinzani wetu kuwa tupo kwenye kinyang'anyiro cha kombe la ligi msimu huu.'' alisema Wenger.
Arsenal wanaialika Swansea inayoorodheshwa katika nafasi ya 16 katika jedwali la ligi ya premia ya Uingereza uwanjani Emirati.


Kichapo hicho cha 3-2 uwanjani Old Trafford hakifai kuwadumaza washika bunduki hao kwani nia na azimio la ni kukata kiu cha kombe la ligi kuu ya Uingereza.


Huku zikiwa zimesalia mechi 9 pekee msimu huu ukamilike kila mechi na alama inaumuhimu mkubwa katika vilabu husika.
Wenger alisema " Kimsingi kichapo hicho kina maana zaidi ya moja kwetu,,,matokeo kamili yatabainika mwisho wa msimu.
Mara ya mwisho Arsenal walipotwaa kombe la ligi kuu ya Uingereza ilikuwa mwaka wa 2004 na hapo jana The Gunners walishindwa kumthibiti tineja Marcus Rashford alifuma kimiani mabao mawili kwa haraka.
Wenger hata hivyo alikataa katakata kukubali kuwa walishindwa na kikosi cha chipukizi cha United.
''tangu lini De Gea amekuwa mchezaji chipukizi, hawa wachezaji waliigharimu United mamilioni ya pauni, Watizame Memphis Depay, Morgan Schneiderlin na Juan Mata hicho ni kikosi dhabiti.''alinuna Wenger


BAADA ya ushindi wa 2-0 jana dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inapanda ndege kwenda kisiwani Pemba kesho kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi ijayo.
Yanga imesonga mbele, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afriuka kwa kuitoa kwa jumla ya mabao 3-0 Cercle de Joachim baada ya awali kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Mauritius.
Sasa mabingwa hao watetezi wanarudi kwenye vita ya Ligi Kuu, Machi 5 wakimenyana na washindani wao wakuu katika mbio za taji, Azam FC.
Zote, Yanga na Azam FC zina pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara – lakini mabingwa watetezi wapo kileleni kwa wastani mzuri wa mabao (GD).
Mchezo wa Jumamosi umebeba taswira halisi ya nani atajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa msimu huu na timu zote zimewekeza katika maandalizi mazuri ndani na nje ya Uwanja.
Azam FC wanakwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndege kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation kesho dhidi ya Panone Uwanja wa Ushirika.
Na Jumanne watarudi Dar es Salaam na moja kwa moja kuingia kambini katika hosteli zao za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF
Februari 24, 2016
Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)
Februari 26, 2016
Ndanda FC 3-0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 
Coastal Union 1-0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
Februari 27, 2016
Mwadui FC 3-1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) 
Prisons 2-1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
Leo; Februari 28, 2016
Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam) 
Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)
Kesho; Februari 29, 2016
Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)


Hamisi Kiiza akimiliki mpira pembeni ya mchezaji wa SIngida United leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

SIMBA SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation baada ya kuifunga SIngida United mabao 5-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam, mabao ya Simba SC yamefungwa na Awadh Juma, Hamisi Kiiza kila mmoja mawili na lingine Danny Lyanga, wakati la Singida limefungwa na Paulo Malamla.
Lyanga ndiye aliyekata utepe wa mabao hii leo Uwanja wa Taifa dakika ya tatu baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na beki wa Singida, Kennedy Juma kufuatia krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. 
Kiiza ‘Diego wa Kampala’ akaifungia Simba bao la pili dakika ya 19, akimchambua kipa Jackton Munna kufuatia krosi ya Tshabalala tena.
Kiiza akafunga bao la tatu dakika ya 66 na la 18 msimu huu tangu ajiunge na Simba kwa kichwa akimalizia krosi ya Mganda mwenzake, Brian Majwega.
Kiungo fundi na asiye na mambo mengi, Awadh Juma Issa ‘Mwana Zanzibar’ akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya 83, baada ya krosi ya Mrundi Emery Nimubona.
Awadh akakamilisha sherehe za mabao za Simba kwa kufunga bao la tano dakika ya 86 akimalizia krosi ya nyota wa mchezo wa leo, Tshabalala wa Manzese.
Mchezo mwingine wa Kombe la TFF leo, Geita Gold inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa Simba, Suleiman Matola imeitoa Toto Africans baada kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Chibuga Chibuga ‘Balotelli’ Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Geita na Simba zinaungana na Yanga iliyoitoa JKT Mlale kwa kuifunga 2-1 Februari 24, Ndanda FC iliyowatoa waliokuwa wanashikilia taji, JKT Ruvu kwa kuwafunga 3-0, Coastal Union iliyoifunga 1-0 Mtibwa Sugar juzi, Prisons iliyowafunga 2-1 Mbeya City na Mwadui iliyowafunga 3-1 Rhino Rangers. 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Justice Majabvi, Jonas Mkude/Peter Mwalyanzi dk77, Awadh Juma, Mwinyi Kazimoto/Mussa Mgosi dk46, Hamisi Kiiza, Daniel Lyanga/Said Ndemla dk61 na Brian Majwega. 
Singida United; Jackton Munna, Paulo Malamla, Adolph Anthon, Kennedy Juma, Hassan Mseka, Abdi Metto/Kassim Hema dk52, Yusuf Kagoma, Songa Jared, Elinywesya Athuman/Yussuf Mfaume dk55 na Yussuf Athuman. 
Powered by Blogger.

Powered by themekiller.com