Watu kadha wameuawa kwenye shambulio la bomu na risasi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Shirika la habari la Reuters linasema watu watatu wamefariki.
Shambulio lilianza kwa ufyatuaji wa risasi na kisha bomu likalipuka polisi walipowasili, afisa wa polisi ameambia shirika la habari la AFP.
Haijabainika ni nani aliyehusika kwenye shambulio hilo.
"Wengi wa waathiriwa ni raia,” afisa wa polisi Ahmed Abdiweli ameambia AFP.
Gavana wa eneo Husayn Ali Wehliye ni mmoja wa waliojeruhiwa, na amepata majeraha madogo kwa mujibu wa vyombo vya habari Somalia.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab limetekeleza mashambulio kadha wiki za karibuni.
Majuzi lilisema lilihusika kwenye shambulio katika hoteli moja mwezi uliopita ambalo liliua watu 15 Mogadishu.
Post a Comment