Halloween party ideas 2015
Showing posts with label Jamii Community. Show all posts


Utawala nchini Malawi umewaondolea mashtaka wanaume wawili waliofumaniwa wakishiriki mapenzi ya jinsia moja, baada ya Uingereza na Marekani kuingilia kati.
Waziri wa sheria nchini Malawi, Samuel Tembenu amesema kuwa mashtaka dhidi yao yameondolewa.
Raia wa Malawi Cuthbert Kulemela na Kelvin Gonani walitiwa mbaroni, na wakahukumiwa na kuzuiliwa kwa muda wa wiki mbili zilizopita, kwa tuhuma za kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Lakini baada ya Marekani na Uingereza kuingilia kati , kwa kuangazia ukikwaji wa haki za binadamu nchini humo, kwa kutumia mitandao ya kijamii na maswali bungeni, mamlaka nchini Malawi imetupilia mbali maashtaka dhidi ya wawili hao.
Waziri wa sheria Samwel Tembenu amesema kuwa mashtaka yao yameondolewa.
Na si hayo tu alisema Malawi inasitisha kwa muda hukumu dhidi yao, wakisubiri matokeo ya sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, ambazo wengi wanasema zimepitwa na wakati.
Mamlaka nchini Uingereza haijathibitisha iwapo ilitishia kusitisha msaada wa pauni 400 inazoipa Malawi kila mwaka.
Malawi imekuwa ikiangaziwa sana kwa msimamo wake mkali kuhusu sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Awali wanasiasa kutoka Malawi waliikemea baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, kwa kile walisema ni kuwasukumia swala la mahusiano ya jinsia moja.


 Wabunge nchini Burundi wameanza mjadala kuhusu hatua ya muungano ya Afrika wa kutuma kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 cha kulinda amani nchini humo, hatua ambayo inafaa kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Hatua hiyo imepingwa vikali na serikali ya rais Pierre Nkurunziza, ikitaja kikosi hicho kuwa cha kigeni kinachovamia taifa hilo.

AU hata hivyo imesema kuwa itasubiri hadi Jumanne kupokea majibu rasmi kutoka kwa serikali ya Burundi.
AU hata hivyo imetangaza kuwa itawapeleka majeshi ya kulinda amani nchini burundi iwe imekubali au imekataa.
Wabunge wanatarajiwa kupinga pendekezo la kutuma kikosi cha kudumisha amani nchini Burundi, kama ilivyopendekezwa na muungano wa Africa.



Chama tawala cha CNDD_FDD kimesema kuwa mjadala huo usiokuwa wa kawaida utakaopeperushwa moja kwa moja kupitia kwa vyombo vya habari, ni wa kuwapa raia sauti kupitia kwa viongozi wao.
Kikosi hicho kitakuwa na kandarasi ya miezi sita ya mwanzo, na ambayo itaendelezwa.
Wanachama 54 wa muungano wa Africa walitangaza siku ya ijumaa kuwa watatuma kikosi cha wanajeshi 5000 kumaliza ghasia zinazoendelea, na ambazo zimeibua hofu ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Naibu msemaji wa rais Jean-Claude Karerwa amesema kuwa Burundi imeweka msimamo wake wazi, haitaki kamwe kikosi cha usalama kutoka nje nchini humo, na kuwa itachukua hatua iwapo kikosi hicho kitatumwa bila idhini ya serikali.
Ongezko la ghasia nchini humo zimeibua hofu ya kutopkea kwa vita vya kiraia, mwongo mmoja baada ya vita vilivyodumu kati ya mwaka wa 1993-2006 kati ya waasi wa kabila la waHutu na majeshi ya watutsi, vilivyosababisha viofo vya watu laki 3.


Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza hali ya hatari nchini humo baada ya shambulio kwenye hoteli moja mjini Bamako kuua watu zaidi ya 20.

Bw keita ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa siku 10, pamoja na siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Watu wenye silaha wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Kiislamu walishambulia hoteli ya Radissom Blue mjini Bamako na kushikilia mateka watu 170.
Maafisa wa Marekani wamethibitisha hakuna mateka zaidi wanaoshikiliwa.
Makundi ya Al-Qaeda Afrika Kaskazini na kundi jingine la al-Murabitoun yamedai kuhusika kwenye shambulio hilo.

Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu shambulio hilo.
Akiongea baada ya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri, Rais Keita alisema watu 21 waliuawa kwenye shambulio hilo, wakiwemo washambuliaji wawili.

Ripoti za awali zilikuwa zimesema watu 27 waliuawa. Afisa wa UN, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema miili 12 ilipatikana ghorofa ya chini ya hoteli hiyo na miili 15 ghorofa ya pili.
Mmoja wa mateka waliouawa ni Geoffrey Dieudonne, mbunge aliyewakilisha jimbo la Wallonia nchini Ubelgiji.
Shirika la habari la serikali ya Uchina Xinhua linasema raia watatu wa Uchina ni miongoni mwa waliouawa. Marekani nayo ilisema raia wake mmoja aliuawa.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond alisema Waingereza watatu waliokuwa hotelini humo wako salama.
Hoteli hiyo inamilikiwa na Wamarekani na hupendwa sana na raia wa kigeni.
Watu walioshuhudia shambulio hilo walisema wapiganaji hadi 13 waliingia kwenye hoteli hiyo wakiimba "Mungu ni Mkubwa!” kwa Kiarabu.
Kabla ya vikosi maalum kuingia humo, mdokezi mmoja aliambia shirika la habari la Reuters kwamba baadhi ya mateka walioweza kukariri vifungu vya Koran waliachiliwa.
Powered by Blogger.

Powered by themekiller.com